Mahakama
Akiongea nje ya Mahakama mara baada ya kusikilizwa kwa shauri hilo Wakili Paul Kisabo amesema Fatma anakabiliwa na shtaka la kubaka kwa kundi kinyume na kifungu cha sheria namba 131A kifungu kidogo cha pili ambacho kinasema anayewasaidia wahalifu kutenda kosa la ubakaji na yeye anahusika kwenye ubakaji wa kundi.
Kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa leo mchana Septemba 5, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu mkazi Dodoma, Fransis Kishenyi lakini badala yake afande huyo alifika mahakamani asubuhi na kusomewa shtaka lake na Hakimu Nyamburi Tungaraja.
Hiyo imekuja baada ya Hakimu aliyepangiwa kusikilizwa kesi hiyo Fransis Kishenyi kuhamishwa kituo cha kazi hivyo Hakimu Tungaraja aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 7 mwaka huu 2024 kwenye mahakama hiyo.
Shauri hilo lililofunguliwa na wakili Paul Kisabo ambaye amefungua mashtaka dhidi ya afande huyo amesema baada ya Hakimu Kishenyi kuhamishwa kituo cha kazi kesi hiyo kwa sasa bado haijapangiwa Hakimu mwingine hivyo Hakimu Tungaraja aliiahirisha tu.