
mmoja asiyejulikana alifika nyumbani kwao, Kigogo Luhanga na kutaka kiroba na mtu mmoja waongozane akabebe ndizi.
Akizungumzia tukio hilo la kusikitisha sana, mama mdogo wa marehemu, Doto Lucas alisema: “Siku ya tukio ambayo ni Alhamisi iliyopita (Machi 12), kijana mmoja ambaye hakuna aliyemfahamu alikuja hapa nyumbani na kumtaka mtu mmoja na kiroba ili akachukue ndizi ambazo kuna mtu aliagiza ziletwe.
“Marehemu ndiye aliyekuwa karibu akijisomea baada ya kutoka shuleni. Mtu mkubwa aliyekuwa nyumbani muda huo ni bibi wa marehemu ambaye ni mtu mzima hivyo alimwambia Irene aongozane na mtu huyo akachukue mzigo akijua uko jirani kwa mujibu wa mtu huyo
“Sisi tuna makaka zetu wakubwa ambao wana kawaida ya kutuagizia mizigo mbalimbali kwenye magari, kwa hiyo tuliamini ni wao. Lakini tulipowapigia simu na kuwaeleza tukio hilo wote walikanusha kuwa si wao na kushangaa.
“Kesho yake asubuhi (Ijumaa) tukasikia kuna binti amekutwa ameuawa kinyama kwenye Bonde la Mto Msimbazi, eneo la Sukita. Tulipatwa na mshituko, tukaenda na kuukuta mwili, tulipoukagua tuligundua ni Irene.
Mungu ailaze roho ya marehemu Irene mahali pema peponi- Amina