Wednesday , 18th Mar , 2015

Star wa muziki Meninah la Lida ametolea ufafanuzi kisa ndani ya wimbo wake mpya wa 'Kaniganda' kinachohusiana na wanawake wawili kugombania mwanaume mmoja, na kukanusha kuwa ni wazo tu na halihusiani na kisa cha kweli katika maisha yake.

Msanii wa muziki wa bongofleva Meninah La Lida

Staa huyo ametoa maelezo haya hasa akihusishwa na uvumi wa yeye katika kipindi cha nyuma kuhusishwa na mahusiano na Diamond Platnumz ambaye tayari ilikuwa ikifahamika kwamba ana mahusiano na Wema Sepetu, kikubwa akiwataka mashabiki wake kukaa tayari kwa rekodi hiyo Jumamosi.