Wednesday , 14th May , 2025

Simba SC kupitia kwa Meneja wa habari na mawasiliano, Ahmed Ally imethibitisha kuwa Nyota wao Elie Mpanzu ni mchazaji halali mwenye mkataba na kikosi hicho wa miaka miwili tofauti na taarifa zilizosambaa kuwa nyota huyo yupo kwa mkopo ndani ya kikosi hicho.

Meneja wa habari na mawasiliano Simba - Ahmed Ally

"Mpanzu ni mchezaji halali wa Simba Sc ambaye amesajiliwa kwa mkataba wa miaka miwili, tayari mwaka mmoja umemaliza ambao ametumikia miezi minne tu baada ya dirisha dogo kufunguliwa kwahiyo Mpanzu bado ana nusu msimu akamilishe mwaka mmoja halafu aje aanze kuitumikia Simba kwa mwaka mwingine mmoja."

"Sisi tunamamlaka naye tukiamua kumuuza, tutamuuza na tukiamua abakie atabakia, hayupo hapa kwa mkopo. Kwa sasa ana miaka 22 na atacheza hapa hata kwa miaka 35 kisha anaweza kuondoka Simba kwenda klabu nyingine ya Tanzania. Kwahiyo wanaomtaka Mpanzu basi wasubiri kama walivyosubiri kwa namba 20 wetu na namba 17 wetu aliyekuja hapa kama kijana mdogo vivo hivo wasubiri kwa Mpanzu"- Ahmed Ally 

Ahmed Ally amesisitiza kuwa Simba imepita level za kumchukua mchezaji kwa mkopo labda atoke Manchester United au Al Ahly lakini pia amesema kuwa "Mchezaji aliyekuwa wao atakuwa wetu na wetu atabaki kuwa wetu"-Ahmed Ally