Monday , 19th May , 2025

Naibu Rais wa Kenya Kithure Kindiki amewahakikishia Wakenya kuwa uchaguzi wa 2027 utakuwa huru, wa haki na wa amani.

Kindiki ambaye alichukua nafasi ya Rigathi Gachagua, Kindiki amewataka wananchi kuwapuuza wanaotabiri ghasia katika uchaguzi huo

Kauli hiyo ya Kindiki inafuatia matamshi ya aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, aliyeonya kuhusu uwezekano wa ghasia iwapo Rais William Ruto atavuruga uchaguzi wa 2027

Akizungumza na wanahabari hivi karibuni, Gachagua alisema kuwa iwapo uchaguzi huo utaibiwa, Kenya itashuhudia ghasia zaidi ya ile iliyoshuhudiwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2007 ambapo maelfu waliuawa katika ghasia za baada ya uchaguzi. 

Kindiki pia amewataka wanasiasa kuruhusu utawala wa Kenya Kwanza kutekeleza majukumu yake badala ya kutumia miaka mingi katika mazungumzo ya kisiasa. 

"Hatuwezi kuwa katika hali ya kudumu ya kampeni. Hata biblia inasema kuna msimu wa kila jambo. Huu ni msimu wa serikali kutoa, wanaojihusisha na siasa hawana lolote la kuwapa Wakenya,"