Wednesday , 21st May , 2025

Bunge la Uganda limepitisha mswada wa sheria kuhusu UPDF, mswada ambao sasa utaruhusu mahakama za kijeshi kusikiliza kesi za kiraia, hatua ambayo imeenda kinyume na uamuzi wa hivi karibuni wa mahakama ya juu ambayo ilisema mahakama hizo hazina hadhi kikatiba kusikiliza kesi za kiraia.

Moja ya marekebisho muhimu yaliyofanywa na bunge ni kulitaka jeshi kuweka alama kwenye vyombo vyao vyote na mavazi ili kuvitenganisha na vile vya raia.

Pia, sasa ni sharti kwa mkuu wa mahakama ya kijeshi kuwa wakili katika cheo cha Jaji wa mahakama kuu na kwamba aliyehukumiwa anaweza kukata rufaa katika mahakama ya juu zaidi ya kiraia.

Sheria hii imepingwa na watetezi wa haki za binadamu na upinzani wekisema kwamba itatumika kuwalenga wakati nchi inakaribia uchaguzi ujao.