Thursday , 12th Jun , 2025

Takriban watoto milioni 138 walitumikishwa katika ajira za watoto mwaka 2024, ikiwemo watoto karibu milioni 54 katika kazi hatarishi ambazo huenda zikaathiri afya, usalama au maendeleo yao.

Ikiwa leo dunia inaadhimisha siku ya kupinga ajira kwa watoto, takwimu hizo mpya zinaonyesha kuwa angalau kiwango cha ajira kwa watoto kimepungua kwa watoto milioni 20 tangu mwaka 2020 ikilinganishwa na kati ya mwaka 2016 hadi 2020.

Licha ya maendeleo hayo, ulimwengu umeshindwa kufikia lengo lake la kutokomeza kabisa ajira kwa watoto kufikia mwaka huu wa 2025. Ripoti hiyo ya mwaka 2024, inatilia mkazo wa kwamba licha ya maendeleo hayo, mamilioni ya watoto bado wananyimwa haki ya kusoma, kucheza na kuwa watoto.

Mkurugenzi mtendaji wa ILO Gilbert F. Houngbo, amesema katika ripoti hiyo kwamba wazazi wenyewe wanapaswa kuungwa mkono na kuwezeshwa kupata kazi za maana ili waweze kuhakikisha kwamba watoto wao wapo madarasani na sio kuuza vitu sokoni au kwenye mashamba ili kuzisaidia familia zao.

Kwa mujibu wa takwimu, sekta ya kilimo ndio inayoongoza katika kuwatumikisha watotokwa asilimia karibu 61, ikifuatiwa na sekta ya utoaji huduma 27% kama vile kazi za majumbani na kuuza bidhaa sokoni huku sekta ya viwanda ikiwemo uchimbaji madini na uzalishaji ikichangia asilimia 13.

Kanda za Asia na Pasifiki zilishuhudia punguzo kubwa zaidi la ajira kwa watoto tangu mwaka 2020, huku kiwango cha ajira kwa watoto kikishuka kutoka asilimia 6 hadi asilimia 3.

Kanda ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara imebakia kubeba mzigo mkubwa, ikiwa na zaidi ya theluthi karibu mbili yaajira za watoto, sawa na watoto milioni 87. Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12 anasimulia sababu iliyomfanya kutafuta kibarua katika maeneo ya kuchimba migodi huko Sierra Leone..