
Pichani ni Mbosso na Mocco Genius
"Mimi nafurahia mafanikio ya Mbosso kwa ujumla haijalishi nimefanya naye wimbo au sijafanya naye wimbo mimi nafurahi tu kuona zake zinaenda vizuri" Amesema Mocco
"Mbosso ni miongoni mwa wasanii ambao utunzi wa nyimbo zake unapendwa na kila mtu,wewe ukitaka kuona kama #Mbosso ni msanii noma na watu ni kama hawampi heshima yake Post picha ya Mbosso na msanii yoyote halafu uliza mtunzi noma nani utaona majibu ya watu, kwahiyo mimi namkubali sana" Amesema Mocco
Mocco amefunguka hayo usiku wa jana wakati msanii Mbosso akifanya uzinduzi na usikilizwaji wa albamu yake mpya Room number 3 ambayo tayari imekwisha toka na inapatikana kwenye mitandao yote ya kusikilizia muziki