Friday , 20th Jun , 2025

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini Seleman Bungara (Bwege) ambaye hivi karibuni alifanya mahojiano na #EastAfricaRadio na kueleza hali yake kiafya hususani changamoto yake ya figo amesema kuwa mtoto wake wa kiume amekubali kumchangia figo moja na tayari ameanza vipimo vya awali kufaniki

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini Seleman Bungara (Bwege) ambaye hivi karibuni alifanya mahojiano na #EastAfricaRadio na kueleza hali yake kiafya hususani changamoto yake ya figo amesema kuwa mtoto wake wa kiume amekubali kumchangia figo moja na tayari ameanza vipimo vya awali kufanikisha jambo hilo

Akizungumza na #EARADIO na #EATV Bwege amesema mtoto wake huyu anayeitwa Haji tayari ameanza vipimo vya awali ili kukamilisha mchakato huo wa kumchangia figo 

Mbunge huyo wa zamani hivi karibuni alizungumza katika mahojiano na Exaud Mtei ambapo alieleza kuwa figo zake mbili hazifanyi kazi na wataalam wamemueleza kuwa mwili wake upo imara kama atafanikiwa kupata figo nyingine atarejea kwenye uimara wake.

Bwege amesema kuwa baada ya mahojiano yale ameendelea kupata msaada wa wadau mbalimbali wakimchangia ikiwemo zoezi ambalo linaendeshwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mohamed Nyundo kuwahamasisha wananchi wa Kilwa kumchangia apate matibabu.

Amesema kuwa viongozi kadhaa wa serikali wameendelea kumchangia ili akamilishe matibabu yake.