Friday , 27th Jun , 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwa mchakato wa kupata Katiba mpya utafanyika katika kipindi kijacho cha miaka mitano.  

 

Akihutubia Bunge muda huu jijini Dodoma katika hafla ya kulivunja rasmi Bunge la 12, Rais Samia amesema Serikali yake itaweka mazingira bora ya kuendesha mchakato huo kwa maridhiano, utulivu na mshikamano wa kitaifa.