Friday , 27th Jun , 2025

Katika hotuba yake ya kulivunja Bunge leo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameeleza baadhi ya mafanikio ya Serikali yake, akitaja kukamilika kwa miradi mikubwa ya kimkakati.

Miongoni mwa miradi hiyo ni Daraja la ambalo lina urefu wa kilomita 3, likiwa miongoni mwa madaraja marefu zaidi nchini na Afrika Mashariki.

Rais Samia amesema mradi huo ni sehemu ya jitihada za kuunganisha mikoa, kukuza biashara na kuimarisha usafirishaji wa watu na mizigo.