Saturday , 28th Jun , 2025

Akitoa nasaha kwa viongozi wapya aliowateua, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemtaka Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi

Mheshimiwa Agnes Meena, kuhakikisha anasimamia kikamilifu mradi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa.

Rais Samia amesema kukamilika kwa bandari hiyo kutazalisha ajira kwa zaidi ya vijana 30,000 nchini, na hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira.