Sunday , 29th Jun , 2025

Arthur Kaluma mwenye umri wa miaka 23 raia wa Marekani na Uganda mara baada ya kupata nafasi ya kuingia mkataba wa mwaka mmoja na vigogo wa mpira wa kikapu ukanda wa Magharibi nchini Marekani, Los Angeles LakerS, imemfanya kuwa mchezaji wa tatu mwenye asili ya Uganda kushiriki ligi hiyo.

Arthur Kaluma amefata nyayo za magwiji wa mpira wa kikapu kutoka Uganda akiwemo Brandon Davies mwenye uraia wa Marekani na Uganda ambaye alicheza NBA kwenye timu ya Brooklyn Nets pia kapita As Monaco iliyopo barani Ulaya alikua MVP mwaka 2018 katika ligi namba mbili kwa ubora Euro league .

Mchezaji mwingine wa Uganda mwenye asili ya Marekani ni Ishmail Carzell Wainwright aliepita kwenye timu mbalimbali nchini Marekani Phoenix Sun, Portland Trail Blazers na Toronto Raptors.

Arthur Kaluma ambaye wazazi wake wote ni raia wa nchini Uganda Patrick Ariko na Saira Ariko alipata rasmi uraia wa nchi hiyo mnamo mwaka 2020 ameichezea timu ya Taifa katika mashindano ya mpira wa kikapu barani Africa Fiba Afrobasket mwaka 2021, pia alijiunga na Timu hiyo kupambania nafasi ya kufunzu kombe la Dunia Fiba word Cup mwaka 2022

Mchezaji huyo mwenye urefu wa futi 6 mpka 7 ambaye jina lake alikuepo kwenye NBA Draft 2025 rasmi amejiunga na Lakers kwa makubaliano ya mkataba wa mwaka mmoja wakiridhisha na kiwango chake wataingia mezani kuongeza miaka mengine.