
Katika mafanikio makubwa katika uwanja wa upandikizaji wa xeno, madaktari wa upasuaji wa China wamefanikiwa kupandikiza pafu la nguruwe kwa mtu ambaye ubongo wake umepoteza uwezo wa kufanya kazi.
Utaratibu huu muhimu, uliofafanuliwa katika jarida la Nature Medicine, unawakilisha hatua ndogo lakini ya kuahidi kuelekea matumizi ya nguruwe waliobadilishwa vinasaba kama chanzo cha kutosha cha viungo vya upandikizaji wa binadamu.
Operesheni hiyo, iliyofanyika mwezi Mei 2024 katika Hospitali ya kwanza yenye uhusiano na Chuo Kikuu cha Matibabu cha Guangzhou, ilihusisha kuchukua nafasi ya pafu la kushoto la mtu wa miaka 39 ambaye alikuwa amepatwa na ugonjwa wa kuvuja damu kwenye ubongo.
Pafu la nguruwe, lililobadilishwa vinasaba ili kuboresha utangamano wake na tishu za binadamu, lilifanya kazi katika kwa mtu huyo kwa siku tisa.
Katika kipindi hiki, kiungo hiki kilibadilish oksijeni na dioksidi kaboni kwa ufanisi, kuonyesha uwezo wake wa kutimiza kazi yake ya msingi.
Maendeleo haya ni ya ajabu hasa kutokana na ugumu wa upandikizaji wa mapafu, hata kati ya wafadhili na wapokeaji.
Wanasayansi wanasema utafiti huo unanuwia kukabiliana na uhaba wa viungo muhimu vinavyohitajika kote duniani kwa matibabu.