Tuesday , 30th Sep , 2025

Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wanasema wamekubaliana mpango mpya wa amani wa Gaza, na kuionya Hamas kuukubali

Mpango huo unapendekeza kusitishwa mara moja kwa operesheni za kijeshi na Hamas kuwaachilia huru mateka 20 wa Israel na wengine zaidi ya 20 ambao wanaaminika kufariki dunia ndani ya saa 72, ili kubadilishana na mamia ya raia wa Gaza wanaozuiliwa.

Chanzo cha Palestina kinachofahamu mazungumzo hauyo kimesema kwamba maafisa wa Hamas wamepewa pendekezo lenye kugusia vipendele 20 la Ikulu ya Marekani.

Moja wapo ya mapendekezo ni kwamba Hamas haitakuwa na jukumu lolote katika kutawala Gaza, na kufungua mlango kwa upatikanaji kamili wa taifa la Palestina.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kufuatia mazungumzo katika Ikulu ya White House, Trump aliutaja mpango huo kuwa "siku ya kihistoria kwa amani".

Lakini alisema kuwa Netanyahu ataungwa mkono na Marekani "kumaliza kazi ya kuharibu tishio la Hamas" ikiwa Hamas haitakubali mpango huo.

Netanyahu kisha akasema Israel "itamaliza kazi" ikiwa Hamas itakataa mpango huo au haitaufuata.