Monday , 27th Oct , 2025

Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. Evaline Munisi ametoa tamko hilo leo, Oktoba 27, 2025 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari makao makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.

Chama Cha NCCR-Mageuzi kimempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiongoza vyema serikali bila kutetereka na kuhakikisha usalama vinadumu nchini licha ya kupata misukosuko kadhaa ya viashiria ya uvunjifu wa amani.

Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk. Evaline Munisi ametoa tamko hilo leo, Oktoba 27, 2025 alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari makao makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam.

NCCR-Mageuzi pia imeongeza kuwa inapinga maandamano ya aina yoyote ambayo yanaashiria uvunjifu wa amani nchini, ambao utaleta taharuki na hofu kwa wapiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu na kuwaasa watanzania kujitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura.

Dk. Munisi amesema katika Ilani yao ya mwaka 2025 ajenda yao nambari moja kati ya ajenda kumi ni Muafaka wa Kitaifa ili kuleta Maridhiano kwakuwa wanaamini amani na mshikamano utaletwa na mwafaka.

Aidha amesema chama hicho kinampongeza Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Fransis Mutungi, kwa kuwa na malezi mazuri kwa vyama vya siasa malezi hayo yamesababisha kampeni kuwa ni tofauti na zilizopita kwakuwa zinaenda kidiplomasia kila mmoja akinadi ilani ya chama chake bila magomvi wala kulumbana baina ya vyama.