Sunday , 28th Dec , 2025

“Katika tukio hilo, Festo steven Maneno (30), mkulima na mkazi wa Mnyika alikamatwa katika shamba hilo akifanya shughuli mbalimbali,”

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro limefanikiwa kuteketeza shamba la bangi lenye ukubwa wa hekta 2.5 katika operesheni ya kudhibiti dawa za kulevya iliyofanyika jana Disemba 27,2025.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro iliyotolewa leo Disemba 28, operesheni hiyo ilifanyika katika eneo la Mnyika, Kijiji cha Chonwe, kata ya Vidunda, Wilaya ya Kipolisi Ruhembe.

“Katika tukio hilo, Festo steven Maneno (30), mkulima na mkazi wa Mnyika alikamatwa katika shamba hilo akifanya shughuli mbalimbali,” taarifa ya Polisi imebainisha.

Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limesema jitihada za kumsaka mmiliki wa shamba hilo, Peter Christian Ngomawenja zinaendelea ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.