Wednesday , 21st Jan , 2026

Malkia wa muziki wa Afrobeat kutoka Nigeria Tiwa Savage, anasema alilia sana alivyojifungua mtoto wa kiume sababu matarajio yake ilikuwa apate mtoto wa kike kwanza.

Picha ya Tiwa Savage akiwa na mtoto wake

Tiwa anasema jambo hilo lilisababisha kukosa muunganiko mzuri kati yake na mtoto wake huyo kwa mwaka mmoja au miwili ya kwanza.

"Kiukweli sikuwa na muunganiko mzuri na mtoto wangu wakiume kwa mwaka mmoja au miwili, kila mara nilitaka mtoto wa kike kwanza nilivyoambiwa amekuja wakiume nilianza kulia". anasema Tiwa Savage

Msanii huyo alijifungua mtoto wake huyo Jamal Balogun mwaka 2015 alipokuwa kwenye ndoa na Tunji TeeBillz.