Thursday , 9th Jul , 2026

Mwenye kiuno bila mfupa Ray C amepiga marufuku kuitwa msanii wa zamani akidai wanaosema hivyo wengi wao wamechelewa kuja mjini.

Picha ya msanii Ray C

Ray C ameandika ujumbe huu akielezea suala hilo juu ya mashabiki na wadau wa muziki kutumia neno la wasanii wa zamani.

"Biashara ya kuitana msanii wa zamani mnitue, na Remmy Ongala mtasema wa lini? King Kiki je? Bi kidude wa mtondogoo au? Semeni tu mlichelewa kuja mjini ndio nishajiamulia" ameandika Ray C