Tanzania, Burundi na DRC kujenga reli ya pamoja

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), alizungumza jambo na Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, Mhe. Nicolas Kazadi (kushoto) na Waziri wa Fedha na Uchumi wa Burundi, Mhe. Dkt. Domitien Ndihokubwayo, baada ya kikao chao na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Kanda ya Afrika Mashariki, Bi. Nnenna Nwabufo (hayupo pichani) kuhusu mkopo wa kujenga Reli ya Kisasa ya pamoja (SGR), katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Washington DC, nchini Marekani.
Nchi za Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimewasilisha maombi ya kupatiwa mkopo wenye masharti nafuu kwenye Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kutoka Uvinza-Msongati- Gitega, yenye urefu wa Km 939, uliokisiwa kugharimu dol