Msukuma ajitosa kuwania uspika wa Bunge
Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Dkt. Joseph Kasheku Msukuma amejitosa kuwania nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya leo Januari 11, 2022, kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Chake cha CCM.