Kwanini hizi ajali zinagusa wanahabari?- Nape
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye, amesema atahakikisha anafuatilia ripoti kutoka jeshi la polisi, itakayotoa taarifa za ukweli ili kujua ni nini kinachopelekea wanahabari kuguswa zaidi pindi ajali za magari ya misafara ya viongozi zinapotokea.