Serikali yaanda mikakati ya kudhamini Golfu Nchini
Mchezaji chipukizi Isack Daudi kutoka Klabu ya Gofu ya Lugalo akikabidhiwa kombe na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Ally Possi baada ya kuibuka mshindi wa jumla mashindano ya Golfu ya NBC Tanzania Open 2021 jijini Dar es Salaam.Katika mashindano hayo mchezaji chipukizi Isack Daudi kutoka Klabu ya Gofu ya Lugalo ameibuka kuwa mshindi wa jumla wa mashindano ya mwaka 2021.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizaraya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Ally Possi usiku wa Desemba 5, 2021 amefunga rasmi mashindano ya Golfu ya NBC Tanzania Open 2021 jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa kanuni za mchezo.