Rekodi zaitesa Mbeya City dhidi ya Simba SC
Kuelekea mchezo wa leo kati ya Mbeya City dhidi ya Simba SC katika dimba la Sokoine, rekodi zimeendelea kuitesa wagonga nyundo wa jiji la mbeya, ambapo katika mechi tano zilizopita, wamefungwa mitanange yote kwa jumla ya mabao 13 huku wao wakifunga magoli mawili tu.

