RC Mongella apiga marufuku mikusanyiko Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella, amesema kuwa kuanzia sasa mikusanyiko isiyo halali mkoani humo itadhibitiwa na kuwataka wananchi kuachana na mikusanyiko hiyo kwa lengo la kujiepusha na maambukizi ya virusi vya Corona.