Majangili wa Tembo wakamatwa
Jeshi la polisi mkoani Simiyu, linawashikilia watu wawili wakazi wa Kijiji cha Longalombogo wilayani Itilima mkoani humo, baada ya kuwakuta na meno mawili ya Tembo pamoja na fuvu lake, wakiyasafirisha kupeleka Kahama mkoani Shinyanga kwenda kuyauza.