Lema akosoa adhabu za bunge
Baada ya adhabu kutolewa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kwa wabunge Halima Mdee wa Kawe na Ester Bulaya wa Bunda mjini, Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amefunguka na kudai kwamba haki imenyongwa kupitia wabunge hao.

