Jumatano , 28th Apr , 2021

Wawekezaji wa vituo vitatu vya mabasi yaendayo Mikoa ya Kusini na maeneo ya shamba vilivyopo mbagala rangi tatu wamesema endapo serikali itakamilisha kwa wakati ujenzi wa miundombinu ya barabara inayoingia katika vituo hivyo itaongeza pato katika kodi zinazolipwa na wafanyabiashara hao.

Muonekano wa Kituo cha Mabasi Mbagala jijini Dar es Salaam.

Ombi hilo limetolewa mara baada ya mwandishi wa EATV kutembelea katika vituo hivyo ambavyo vimepewa kibali Cha kutoa huduma hiyo ikizungumza pia na wawekezaji wasimizi ambao wametamani kuziina Taasisi za serikali zikifika hapo kumaliza chochoko choko za kiutendaji zilizo chini ya uwezo wao.

"Magari yote kutoka hapa kwenda maeneo ya pembeni mwa mji huanzia hapa na tunachokifanya ni kuhakikisha abiria wetu wote wanapewa huduma stahiki", amesema Cheche.

Awali Msimamizi wa stendi namba 21 amesema serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imewapa dira na ujasiri  wawekezaji wa ndani hivyo akiwakumbusha watanzania kuwa awamu za ujanjaunjanja hazipo tena Tanzania.

"Sisi hapa tunafanya Kazi bila tatizo sema na sisi ndo tinaamua utoe Kituo gani Ili abiria wako wapate unafuu usalama wa mizigo yao"aamesema Chacha.