DSTV yaja na tia vitu pata vituz

Jumanne , 21st Jan , 2020

Kampuni ya Multichoice Tanzania DSTV, imetangaza kampeni ya ofa yao mpya inayokwenda kwa jina la tia vitu pata vituz, ambayo itamrahisishia maisha Mtanzania na mteja wa huduma zao.

Kutoka kushoto pichani ni Mkuu wa kitengo cha masoko Multichoice Tanzania Baraka Shelukindo, msanii wa filamu na muziki Jacqueline Wolper, Dully Sykes na mkuu wa kitengo cha thamani kwa wateja Hilda Nakajumo

 

Ofa hiyo imezinduliwa rasmi siku ya leo Januari 21, 2020, Jijini Dar es Salaam, na kwamba mteja wa kifurushi cha Bomba, akilipia shilingi 19,000 atapatiwa nyongeza ya kifurushi cha Family chenye thamani ya shilingi 29,000.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Hilda Nakajumo, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Thamani kwa wateja kutoka Multichoice Tanzania ameeleza kuwa,

"Mteja wetu wa kifurushi cha bomba akilipia shilingi 19,000 anapatiwa kifurushi cha family chenye thamani ya shilingi 29,000 bure ndani ya mwezi mzima, ofa hii tuliianza Januari 15 na tumeona maendeleo yake ni mazuri, lakini tumewaita wadau wetu wa habari ili waweze kutufikishia kwa wingi zaidi kwa  watanzania wengine wajue ili wanufaike kwa pamoja" amesema Hilda.

Aidha Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Baraka Shelukindo, ameongeza kusema "Tia vitu pata vituz ni muendelezo wa mambo ambayo tumekuwa tukiyafanya siku zote kuangalia wateja wetu, watanzania wenzetu kwamba tunawapa ahueni au vitu gani vizuri  ili waweze kuishi kwa furaha"