Serikali yawapa siku 90 wajasiriamali

Jumanne , 4th Sep , 2018

Wajasiriamali wanaozalisha bidhaa mbalimbali nchini wametakiwa ndani ya miezi mitatu, kuhakikisha wanathibitisha ubora wa bidhaa zao na atakayekiuka hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Picha ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali

Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa shirika la viwango nchini TBS Dkt. Yusuf Ngenya, wakati akifungua semina kwa wajasiriamali wanaotengeneza bidhaa mbalimbali nchini jijini Dodoma.

Amesema kwa kutambua bidhaa nyingi nchini zinazotengenezwa na wajasirimali zilizopo sokoni hazijathibitishwa kwa ubora wa viwango hivyo shirika hilo limeamua kufanya semina ili kuwasaidia wajasirimali kuweza kupeleka bidhaa zao katika maabara ya TBS na kupatiwa vibali vya ubora.

Aidha Dk. Yusuf amesema wameingia makubaliano na shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo nchini sido kwa wao kuwasimamia wajasiriamali na kuwapa barua na kwenda TBS kuweza kupata kibali.