TBS kujiendesha kidijitali sasa

Ijumaa , 30th Apr , 2021

Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Shirika la viwango Tanzania TBS limewataka wadau, wateja kutumia huduma mpya ya kielektroniki, mfumo ambao umepewa jina la viwango jumuishi, uhakiki wa ubora, ugezi na upimaji yaani ISQMT.

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango TBS Dkt Athumani Ngenya

Akizindua Mfumo huo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Viwango TBS Dkt Athumani Ngenya sambamba na Mkurugenzi wa Trade mark East Africa John Ulanga wameeleza kuwa Mfumo huo utapunguza muda na gharama kwa wadau na wateja kulazimika kufika ofisi za TBS kupata huduma zinazolazimika na udhibiti wa ubora,v iwango uchukuaji wa vibali na vyeti.

"Zamani wadau ilikuwa ikiwalazimu kusafiri umbali mrefu kuchapisha  nyaraka ama kuwasilisha. Maombi kwenye makaratasi mchakato ambao ulitawaliwa na makosa na ucheleweshaji," amesema Dkt Athumani.

Aidha amesema ni wakati muhimu sasa kwa wadau hususani wazalishaji waingizaji wa bidhaa mbali mbali kutumia Mfumo huu Ili kurahisisha utendaji kuelekea kasi ya Tanzania ya Viwanda  yenye uchumi wa Kati wa juu.

"Utoaji wa huduma za kidijitali umepungiza gharama na muda wa kufanya biashara hivyo kurahisisha ufikiwaji wa malengo ya ukuzaji Viwanda na maendeleo ya uchumi nchni Tanzania" amesema Dkt Athumani