Jumanne , 24th Jan , 2023

Shirika la mafuta la serikali ya Uganda limesema kwamba, nchi hiyo  itaanza kuchimba kisima chake cha kwanza cha mafuta katika eneo la mafuta la Kingfisher, siku ya leo.

Inatarajiwa kuwa ifikapo mwaka 2025 mapipa ya kwanza ya mafuta yenye uwezo wa kufikia bilioni 1.4 yatasukumwa kutoka visima katika eneo la katikati ya magharibi.

Mamlaka ya Mafuta ya Uganda (PAU)imesema kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kwamba, jumanne ya leo inakwenda kuwa hatua  nyingine muhimu na kusogeza hatua karibu na mafuta ya kwanza kwa uzinduzi wa uchimbaji na uzalishaji wa   mafutadeleo .

Rais Yoweri Museveni anatarajiwa kufanikisha hafla hiyo. Shughuli za uchimbaji mafuta  huko Kingfisher zinaendeshwa na kampuni ya  CNOOC ya China, huku eneo la Tilenga zikiendeshwa na kampuni ya Total Energie ya Ufaransa.