Wageni walitawala soko Tanzania

Jumanne , 25th Feb , 2020

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja Miradi wa Soko la Hisa la Dar es Salaam, Emmanuel Nyalali, imeeleza kuwa juma lililoishia Februari 21,2020, wawekezaji wa nje walichangia asilimia 93.41ya thamani ya mauzo yote ya hisa na asilimia 95.80 ya thamani ya manunuzi yote ya hisa.

Mchoro unaoonesha mnyororo wa thamani

Nyalali amesema kuwa kwa mwaka huu wa 2020, wawekezaji wa nje wameshachangia asilimia 87.40 ya thamani ya mauzo ya hisa na asilimia 93.46 ya thamani ya manunuzi ya hisa.

Akitoa taarifa ya mauzo ya hisa kwa juma lililoishia Februari 21, 2020, Nyalali amesema jumla ya hisa milioni 6.85, zenye thamani ya Shilingi bilioni 19.28, ziliuzwa na kununuliwa sokoni, ikilinganishwa na mauzo ya hisa milioni 1.40 zenye thamani ya Shilingi Milioni 472.44, zilizouzwa kwa juma lililoishia Februari 14, 2020.