Jumapili , 16th Jun , 2019

Mkazi wa Misungwi Mkoani Mwanza William Mathias amewaomba wasamaria wema kujitokeza kumsaidia kupata matibabu kutokana na tatizo la kutoona ambalo linamkabili.

William Mathias

Akizungumza na Kurasa ya EATV leo Jijini Dar es Salaam, William ambaye amefika kwa ajili ya matibabu amesema tatizo la kutoona limekuwa likimsumbua na kushindwa kukidhi mahitaji yake.

Tatizo hilo linalomkabili, limedumu kwa kipindi cha miaka 34 sasa, huku ndugu wanaomhudumia wakielezea changamoto nyingi ambazo wanapitia katika malezi yake.

Tazama hapa chini akizungumza.