Jumapili , 11th Aug , 2019

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Watanzania hawana budi kujifunza kupitia tukio la ajali ya lori iliyopelekea vifo vya Watanzania zaidi ya 60.

Waziri Kangi Lugola ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na EATV na EA Radio akiwa mkoani Morogoro, ambapo amesema pindi ajali za namna hiyo zinapotokea, wananchi hawana budi kuviachia vyombo vya ulinzi na maafa kushughulika na masuala hayo.

"Tukio hili sio la kwanza kutokea na kujifunza, ila niseme Watanzania hatuna budi kujifunza, matukio ya namna hii yanayopotokea tuviache vyombo vya usalama na majanga ya ajali viendelee kushughulika, sisi wengine tukae pembeni", amesema Lugola.

"Nawaomba Watanzania tuendelee kuwa na utamaduni wa kuwa na heshima na tuna sheria ya mitandao, sisi kama Serikali licha ya kukemea tutaendelea kufuatia wakina nani ambao wanaendelea kuzisambaza picha zizizofaa mtandaoni", ameongeza.

Mapema leo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amefika mkoani Morogoro kwa ajili ya kushiriki mazishi ya watu waliopoteza maisha kwa ajali hiyo.

Fuatilia mahojiano kamili hapo chini.