
Mwanamke aliyekatwa na mpenzi wake
Akizungumza hii leo Oktoba 11, 2022, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng'anzi, amesema tukio hilo limetokea wilayani Magu katika msitu wa Sayaka ambapo mwanaume huyo anadaiwa kumchukua mpenzi wake huyo na kutekeleza unyama huo kisha kukimbia kusikojulikana.