Jumatatu , 21st Oct , 2019

Hatimae upelelezi wa kesi inayomkabili mfanyabiashara Khamis Said, anayedaiwa kumuua na kisha kumchoma na moto wa magunia mawili ya mkaa mke wake Naomi Marijani, na kisha mabaki ya mwili huo kwenda kuyafukia shambani kwake Mkuranga umekamilika.

Akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Wakili wa Serikali Wankyo Simon, amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekwishakamilika na kwamba upo katika hatua za mwisho za uchapishwaji ili jalada hilo lipelekwe Mahakama Kuu.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkuu wa Mahakama hiyo Salumu Ally, aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 4, 2019.

Mshtakiwa huyo anadiwa kutenda kosa hilo Mei 15, 2019, nyumbani kwake maeneo ya Gezaulole Kigamboni.