Jumanne , 17th Jan , 2023

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Angellah Kairuki amesema hajaridhishwa na hali ya asilimia 55.2 ya wanafunzi waliotakiwa kujiunga na kidato cha kwanza mkoani Tanga kutoripoti shule

Waziri Kairuki ametoa kauli hiyo mkoani Tanga wakati akizungumza na Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule za  Sekondari, Walimu Wakuu wa Shule za Msingi  na viongozi wa Elimu ngazi ya Halmashauri kwenye kikao kazi cha Uboreshaji wa Usimamizi wa Elimumsingi na Sekondari katika shule ya sekondari Tanga ufundi

Amesema takwimu za wanafunzi walioripoti kidato cha kwanza si ya kuridhisha katika mkoa huo.

“Kwa upande wa uwandikishwaji Wanafunzi darasa la kwanza mmefikia asilimia 87.7 lakini changamoto inakuja kwenye kuripoti Wanafunzi wa kidato cha kwanza, mpaka Januari 13, mwaka huu zaidi ya Wanafunzi 27,867 ambao ni sawa na asilimia 55.2 hawajaripoti Shule” amesema Waziri Kairuki

Aidha Waziri Kairuki ametaka watoto wenye ulemavu kupewa kipaumbele katika uandikishwaji

“Ukiangalia kwenye elimu ya awali mpaka sasa uandikishwaji ni asilimia 82, lakini nilitamani nisikie kwa upande wa wanafunzi wenye mahitaji maalum ni asilimia ngapi ili nao tusiwaache nyuma"