Jumatano , 21st Sep , 2022

Rais Macky Sall wa Senegal  ametoa wito wa kuondolewa vikwazo dhidi ya nchi ya  Zimbabwe kwenye mkutano wake wa 77 wa umoja wa mataifa huko New York.

Kiongozi huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Umoja wa Afrika mesema kwamba vikwazo dhidi  Zimbabwe vinawatesa wananchi  wa Taifa hilo.

Marekani na Umoja wa Ulaya (EU) wanaendeleza vikwazo dhidi ya Zimbabwe, sababu zikielezwa kwamba ni ukosefu wa demokrasia nchini humo,ukosefu wa haki za kibinadamu na ukosefu wa uhuru wa habari.  

Vikwazo hivyo vinawalenga moja kwa moja Rais wa Taifa hilo Emmerson Mnangagwa na taasisi zake.

Uchumi wa Zimbabwe umekua kwenye hali ngumu ndani ya miongo kadhaa iliyopita ukiathiriwa na mfumuko mkubwa wa bei huku hali hiyo ikisemekana kuchangiwa na vikwazo.  

Rais Sall ni kiongozi wa kwanza kutoka barani Afrika kuhutubia Mkutano mkuu wa UN. Amelitaka baraza la usalama la umoja wa mataifa kuiangazia migogoro inayojiri barani Afrika kama migogoro ya nchi zingine.

 Pia ametaka Afika ipewe kiti kwenye kundi la nchi 20 (G20) ambalo linaundwa na nchi 20 duniani zenye uchumi mkubwa.
Viongozi wengi wa Afrika wanatarajiwa kutoa hotuba  zao kwenye mkutano huo hii leo.