
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, na Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina
Kauli hiyo imekuja baada ya Mbunge huyo kudai kwamba mfumuko wa bei za mbolea ni wa kutengeneza kwa manufaa ya wafanyabiashara na kutaka takwimu za bei ya mbolea walizonazo serikali waziangalie
"Ni hatari kwenye capacity ya mtu ambaye ni mbunge wa muda mrefu amekua Naibu Waziri na Waziri kusimama bungeni na kuzungumza issue ambayo totally he is misleading the public, bei ya mbolea duniani si jambo la kuficha, hata uki-google unazipata bei, nimuombe Mh.Mpina kama ana-source yoyote ya kunipatia mbolea ya bei rahisi aje nampa mkataba wa Tani laki nne zote aniletee,"amesema Waziri Bashe