Jumatatu , 9th Nov , 2015

Baraza la vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo BAVICHA wamesema kuwa wameamua kuingilia kati kushawishi suala la utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa wao kuitisha mgomo nchi nzima.

Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la CHADEMA,(BAVICHA), Julius Mwita

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la CHADEMA,(BAVICHA), Julius Mwita leo jijini Dar es salaam wakati ikiongea na waandishi wa habari katika ofisi za CHADEMA katika kuelekezea msimamo wa vijana wa chama chao juu ya mikopo ya elimu ya Juu.

Mwita ameongeza kuwa wametoa masaa 72 endapo Serikali isipotekeleza suala la ukamilishaji wa utoaji mikopo hiyo basi kwa kuwa BAVICHA kimeenea nchi nzima basi watafanya kila njia ili kuanzisha mgomo wa wanafunzi hao ambao hautakuwa na madhara kwa watu wengine.

Kwa upande wake Mratibu Uhamasishaji wa BAVICHA, Edward Simbeye amedai kuwa chama chao kimejiandaa kudai demokrasia nje ya boksi ya kura kutokana Uchaguzi mkuu uliopita kujaa Ulaghai wa Demokrasia.