Alhamisi , 13th Oct , 2022

Mji mkuu wa China , Beijing upo kwenye hali ya sintofahamu ukiwa chini ya ulinzi mkali na kanuni za UVIKO 19 zikizingatiwa  kuelekea mkutano mkuu wa chama tawala cha Kikomunisti nchini humo. 

 

Mamlaka zimezuia watu kuingia jijini humo, huku wasafiri wengi wakizuiwa safari zao . 

Inasemekana wengine waliolazimisha safari zao wamewekwa karantini. 

Hali hiyo imesababisha hasira kwa wakazi  haswa kwenye mitandao ya kijamii na mandamano madogo yakitajwa kuchukua nafasi.

Maandamano yanafanyika katika daraja la Kaskazini Magharibi mwa Beijingi katika wilaya ya  Haidian  

Mabango ya waandamanaji wengi yanataka uhuru wa kisiasa.