Jumatano , 2nd Jun , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba ameamua kumuita Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila jina la petroli kwa sababu ni mlipukaji, kauli ambayo ilimfanya Chalamila aangue kicheko kwa muda mrefu.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Albert Chalamila, akicheka mara baada ya kuambiwa yeye ni mlipukaji

Hayo yamejiri mapema hii leo Juni 2, 2021, Ikulu ya Chamwino Dodoma, wakati akizungumza na viongozi wateule mara baada ya kuwaapisha, na kueleza kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza Ngusa Samike yeye ni kiberiti kwa sababu ni mkimya lakini ana mambo yake katika utendaji.

"Nimewasimamisha kila RC na RAS wake kama alivyosimama Mkuu wa mkoa wa Mwanza nikasema kibiriti na petroli huyu Ngusa ni mkimya lakini ana zake yule kule (Chalamila) mlipukaji sasa sijui huko kutakuwaje lakini tunawaangalia," ameeleza Rais Samia.