Jumanne , 12th Jul , 2016

Fulsa mbalimbali zinazojitokeza nchini kutoka kwa viongozi wa nchi za nje ambao wanakuja nchini kwa lengo lakushirikiana kiuchumi ni lazima serikali iweke chombo chakufanya tathimini kwa ahadi mbalimbali zinazotolewa.

Akizungumza na East Africa Television mtaalamu mtafiti na mshauri wa maswala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Prof.Prosper Ngowi amesema ikiwa ni siku chache baada ya Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kutembelea nchini kwa lengo lakubadilishana mambo mbalimbali na Tanzania hasa kwa masuala ya kukuza uchumi wa nchi ni vema seriklai ikazingatia swala la ufwatiliaji wa ahadi hizop zinatekelezwa kwa namna gani.

Prof.Ngowi amesema kukiwa na tathimini hiyo itasaidia sana taifa kujua vitu gani vyapewa vipaumbele katika kukuza uchumi wa nchi na taifa kufikia malengo ya miaka mitano ambayo ni kuwa taifa la uchumi wa kati.

Kwa upande wao wadau wa maendeleo nchini wamesema fulsa mbalimbali za uwekezaji zilizojitokeza ni vema serikali ikawapa ushirikiano wakaribu ili kuziendeleza fulsa hizo.