Jumatatu , 2nd Jan , 2023

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 9 kujeruhiwa  baada ya helikopta mbili kugongana angani karibu na Seaworld kwenye pwani ya Australia ya Gold Coast

Ofisi ya Usalama wa Usafiri wa angani ya Australia (ATSB) imethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa uchunguzi wa kubaini chanzo chake umeanza

Idara ya polisi ya nchi hiyo imeeleza kuwa helikopta moja ilikuwa ikipaa na nyingine ilikuwa inajiandaa kutua