
Katika enzi zake za kusakata kabumbu Weah amewahi kupata mafanikio mengi makubwa akivunja na kuweka rekodi mbalimbali ikiwemo kuwa mchezzjai pekee kutoka Afrika kushinda Tuzo ya Mchezaji bora wa dunia.
Katika miaka ya 1989, 1994 na 1995, Weah alishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika. Mwaka 1994 George Weah alitwaa kiatu cha dhahabu kwa kuwa mfungaji bora wa ligi ya mabingwa barani Ulaya (UEFA).
Mwaka 1995 ndio ulikuwa mwaka wenye mafanikio kwa Weah na historia kwa bara zima la Afrika baada ya nyota huyo ambaye amewahi kuchezea Monaco chini ya kocha Arsene Wenger alitangazwa kuwa mchezaji bora wa Dunia (FIFA World Player of the Year).
Disemba 20 mwaka 2014 Weah alishinda kuwa Seneta wa jimbo la Montserrado kabla ya kuwania tena nafasi ya Urais kwenye uchaguzi wa mwaka huu ambapo leo asubuhi ametangazwa rasmi kuwa Rais wa 25 wa Liberia.
Weah pia alitwaa tuzo ya Fair Play mwaka 1996 inayotolewa na shirikisho la soka la kimataifa FIFA kwa kumtambua mchezaji muungwana zaidi uwanjani. Mwaka huo huo pia Weah alitangazwa kama mchezaji bora wa Karne ya 19 barani Afrika.