JPM aeleza kilichowakuta Mainjinia Sumbawanga

Jumatatu , 7th Oct , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli, amesema moja ya changamoto alizokumbana nazo wakati wa Ujenzi wa barabara, mkoani Rukwa ni kwa Mainjinia wake kujikuta wamelala nje ya maeneo ambayo walikuwa wamelala usiku, na kueleza hali hiyo ilipelekea kuwakatisha

ujenzi wa barabara.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyoakia mkoani Rukwa alipokuwa akihutubia wananchi wa Sumbawanga kwenye Uwanja wa Nelson Mandela na kusema mkoa huo zamani walikuwa wakilalamika kutengwa.

Rais Magufuli amesema kuwa "kuna wakati fulani Mainjinia wangu niliwatuma wakalala kwenye Makalavati na walipoamka saa 4 asubuhi wakajikuta wako nje, hii ndiyo Rukwa."

Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa "wananchi wa Sumbawanga walikuwa wakilalamika wametengwa aisee ni kweli, nilikuja Sumbawanga miaka hiyo barabara nyingi sana zilikuwa ni changarawe, naomba tuwapongeze Mzee Mkapa na Mzee Kikwete."

Kwa sasa Rais Magufuli, yupo ziarani mkoani Rukwa ambapo ameanzia mkoani Songwe.