Jumatatu , 16th Sep , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa kauli ya kwanza, tangu kuchaguliwa kwa Mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ambaye amechukua nafasi ya Tundu Lissu.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi rada mbili za kuongozea ndege, ambapo amesema jimbo hilo lilikuwa halina mwakilishi.

Rais Magufuli amesema kuwa "nimefurahi kumuona Mbunge wa CUF, lakini nimefurahi kumuona Mbunge ambaye jimbo lilitelekezwa lililokuwa la Tundu Lissu (Miraji Mtaturu), ameingia na kazi, saa nyingine majimbo yanakosa uwakilishi."

"Siku ile ulitoa maagizo Spika tushughulikie tatizo la maji kule, nakuahidi tutashughulikia maji katika jimbo lile (Singida Mashariki) ili yale yaliyochelewa yakamilike kwa haraka haraka." ameongeza Rais Magufuli

Hivi karibuni Bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai alimuapisha Miraji Mtaturu kuwa Mbunge wa Singida Mashariki