Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Liberatus Sabas.
“Mfano, Mkoa wa Mbeya katika wiki mbili wamekufa watu 40, majeruhi zaidi ya 100, hakuna hatua zinazochukuliwa hata ya kuwambia RPC na RTO asijiuzulu. Au hadi wafe wangapi? Mpunguzie hata nyota ili ajue damu za watu zinavyouma. Kaanze na RPC Mbeya”, moja ya kauli ya Magufuli.
Alfajiri ya leo Julai 5, 2018, Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es salaam kimezindua Operesheni ya Ukaguzi wa magari, madereva, leseni na vyeti vya udereva kwa madereva wa mabasi ya Mikoani katika stendi kuu ya Ubungo .
Zoezi hilo limeongozwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Liberatus Sabas, ambapo amesema kuwa lengo la operesheni hiyo ni kuwafanya madereva kuacha tabia ya kughushi leseni, kuwahimiza wajiunge na mafunzo ya udereva katika vyuo vinavyotambulika na serikali.

Mmoja kati ya maaskari walioendesha oparesheni hiyo akikagua gari.
“Polisi Kanda Maalum Dar es salaam inawataka Madereva wasio na leseni halali, madereva walevi, pamoja wamilki wa magari walio na magari mabovu kutoyaruhusu magari hayo kuingia barabarani hadi yatakapotengenezwa na kukaguliwa”, amesema Kaimu Kamanda.
Kamanda ameongeza kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wamiliki, Madereva na Kampuni za usafirishaji zitakazoenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za usalama Barabarani.



