Jumatatu , 5th Oct , 2015

Mwanasiasa mkongwe na muasisi wa chama cha mapinduzi CCM mzee Kingunge Ngombare Mwiru leo ametangaza rasmi kuachana na chama chake alichokitumikia kwa muda mrefu kwa madai ya ukiukwaji wa demokrasia ndani ya chama hicho.

Mwanasiasa mkongwe na muasisi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mzee Kingunge Ngombare Mwiru.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, jana alasiri, Mzee Kingunge amesema hafikirii kujiunga na chama chochote cha siasa baada ya kushiriki harakati za kisiasa na kijamii kwa takribani miaka sitini na moja sasa.

Hata hivyo Kingunge ambaye amekuwa ndani ya chama kwa muda wa miaka 61 amesema hafikirii kujiunga na chama kingine cha siasa na kuwa yeye ni raia huru mwenye haki zake za kisiasa na kijamii na taendelea kuwa na msimamo kuhusiana na masuala ya maendeleo.

Kwa mujibu wa mzee Kingunge, anachukua uamuzi huo wakati nchi ikiwa katika vuguvugu la watu kutaka mabadiliko kutoka kwa makundi yote katika jamii na kwamba yeye anaunga mkono mabadiliko hayo kwani wanaoyataka wana sababu za msingi.